Mahindi Ya Sumu | Maisha Sasa

Wataalam wa afya na maswala ya kilimo wameelezea hofu yao kuhusu ongezeko la matumizi ya kemikali fulani na dawa ghushi inayotumiwa na wakulima kukausha mahindi ghafla ili kwa nia ya kupata viwango hitajika sokoni. Wataalamu wanasema matumizi ya kemikali hii ni kuhatarisha usalama wa chakula. Mwanahabari wetu Gabriel Kudaka na mpiga picha Kenrob Sigei, walizuru bonde la ufa pamoja na kaunti zilizoko mpakani mwa Kenya na nchi jirani za Uganda na Tanzania, na wanatufahamisha jinsi biashara hii inavyotekelezwa.
« | »
News Features