Simulizi Ya Joshua Okaya

Rais wa baraza la wanafunzi chuo cha uwakili cha KSL Joshua Okayo alitekwa nyara tarehe ishirini na sita mwezi jana punde tu baada ya kushiriki maandamano yaliyofikishwa hadi kwenye bunge la kitaifa na la seneti. Akiwa mateka wa maafisa wa usalama, kwa zaidi ya saa 48, Okayo aliteswa kwa kupigwa na vifaa butu, akanyimwa chakula na hatimaye akatupwa kando ya mto Maragua. Katika mahojiano ya kipekee na mhariri wetu Frederick Muitiriri, Okayo ameiambia NTV kwamba maafisa hao walikuwa na nia ya kumuua.

« | »
News Features