KISIIrani: Arati vs Osoro

Kaunti ya Kisii inashuhudia dhoruba kali, kivumbi, na mvutano kati ya gavana Simba Arati na kiranja wa wengi kwenye bunge la kitaifa Silvanus Osoro. Wanasiasa hao ambao zamani walikuwa na ukuruba sasa ni mahasimu. Lakini chanzo cha uhasama wao ni upi? Uadui huu umeibua masuali na minong’ono huku ubabe wa kisiasa kati ya Kenya Kwanza na Azimio la Umoja ukionekana kama chanzo cha uhasama. Hata hivyo wanakandarasi ambao wanasema walishamaliza kandarasi tofauti wana hasira wakidai malipo yao, Osoro akionekana kuwa mtetezi wao naye gavana Simba Arati akisistiza kwamba sharti sheria ifuatwe ya malipo. Mwanahabari wetu wa masuala ya siasa Melita Ole Tenges alifika kaunti hiyo na kuzungumza na viongozi hawa akiangazia kisiirani Kisii.
« | »
News Features