Samia Suluhu aondoa marufuku yakufanya siasa hadharani kwa upinzani
Hatua ya kukubali mikutano ya hadhara ya kisiasa nchini Tanzania imeangaziwa katika vyombo vya habari nchini humo na vilevile kimataifa huku wengi wakiipongeza na kutaja kwamba ni mwamko mpya wa siasa za vyama vingi huko. Baadhi ya washikadau wamefurahia hatua hiyo ya rais Samia suluhu na kuahidi kufanya vikao vingi na wanachama wao huku wengine wakionyesha kuwa na hali ya kutotaka kuweka imani yao kwa maamuzi hayo kwa asilimia mia moja.
Ni katika kikao cha mwanzoni mwa mwaka huu ambapo Rais wa tanzania Samia Suluhu , alikutana na baadhi ya vyama vya kisiasa nchini humo na kutangaza kwamba moja wapo ya vikwazo vilivyowekwa na serikali ya zamani dhidi yao imebatilishwa.
Akitoa nafasi hiyo ambayo wataalamu wa siasa wanasema ni mwanzo tu wa kuboreka kwa siasa za vyama vingi nchini humo, Rais huyo alionya dhidi ya siasa chafu zinazosheheni matusi na kudunishana hadharani.
Baadhi ya wadau wamepongeza hatua hiyo na kutaja kwamba ni mwanzo wa msimu mpya ambapo kila mtanzania anamatumaini kushiriki siasa anazokubaliana nazo bila ya kudhulumiwa.
Wengi wanatarajia kwamba mikutano kama hii ya hadhira itakuwa hali ya kawaida, huku uhuru wa kukutana na kuzungumzia sera zao kisiasa ukikosa kukandamizwa.
Uhuru wa kushiriki demokrasia ya vyama vingi pia ni jambo ambalo wengi wanahisi linapaswa kupendekezwa.
Kwa wale ambao wamebanwa na serikali ya nchi hiyo kwa msimamo wao wa kisasa kama FreeMan Mbowe wa Chadema, hatokuwa mwepesi kupongeza matukio yanayoendelea nchini humo akisisisitiza kwamba demokrasia ingali ina safari ndefu, Tanzania.
Rais Samia amenyoshea mkono wa amani upande wa upinzani tangu kuingia kwake madarakani. Kikao chake ughaibuni na mbunge wa zamani wa Singida Tundu Lissu, kilipokelewa vyema nchini humo huku wengi wakiwa na matumaini kwamba ataweka hali ya usalama wa wanasiasa nchini humu iwe kipau mbele.
Lissu alinusurika kifo baada ya kufyatuliwa risasi 38 nchini Tanzania, akakimbilia kenya kwa matibabu kabla ya kukimbilia Ubelgiji kuishi huko..aliyekuwa mbunge wa arusha Godbless Lema pia alikimbilia ughaibuni akitoroka hali ya usalama wake na familia yake.
Wengi kama Mbowe walikamatwa kwa tuhuma za ugaidi na kupanga mikutano iliyotajwa kama kinyume na sheria.
Kwa miaka saba, vikao vya kisiasa vilikuwa vimepigwa marufuku nchini humo, huku vyama vikuu vya upinzani kama ACT Wazalendo na Chadema vikizuiliwa huku chama tawala kikipata fursa ya kupiga kammpeni zake bila ya matatizo.
Katika uchaguzi wa 2020, amri hiyo ilisimamishwa kwa mda, japo wengi walilalamikia kuvurugwa na idara za usalama.