Kiwewe cha nyuklia

Mpango wa kenya kujenga kinu cha kuzalisha nishati ya nyuklia kitakachokuwa ni cha kwanza kanda ya afrika mashariki na kuwa taifa la pili baada ya afrika kusini waonekana kukaribia kukamilika. Hata hivyo, wenyeji wa kijiji cha uyombo kaunti ya kilifi wanaoungwa mkono na wanaharakati wa mazingira, mashirika ya umma hali kadhalika makundi ya kuhifadhi mazingira wanapinga mradi huo kwa misingi kwamba ni hatari kwa afya, mazingira na pia sekta ya utalii. Je, wanazo sababu tosha kuupinga mradi huo? Wataalamu wa nyuklia wanasema vipi na msimamo wa serikali ni upi? Haya ni makala maalum kiwewe cha nyuklia naye Duncan Khaemba
« |
News Features