Kisirani Kasipul

Mauaji ya mjumbe wa Kasipul Charles Ong’ondo Were kwenye mzunguko wa makafani ya City hapa jijini Nairobi  yalianika bayana kisirani na taharuki ambayo imezidi kutanda kwa muda katika eneo bunge hilo.

Habari zilizochipuka usiku huo na siku chache baadaye baada ya mbunge huyo kuuwawa zilitoa taswira ya eneo bunge lililojaa chuki na kisirani kisiasa.baadhi ya watu wamepoteza maisha, wengine kuumizwa vibaya na wengine wameponea chupu chupu.

NTV imezama Kasipul kujua kiini cha kisirani na utasi huu usiokoma kwenye makala maalum yalyoandaliwa na mwanahabari wetu Duncan Khaemba.

Ila tungependa kuwatahadharisha watazamaji kwamba baadhi ya picha kwenye makala haya huenda zikaogofya.

« |
News Features