Jela Ya Tiba

Kulazwa hospitalini kwa minajili ya matibabu ni tukio ambalo huwatoa wengi kijasho chembamba kutokana hali kwamba hospitali kwa kawaida ni vituo vya kuangazia dharura za kiafya ziwe ni zile hali mahututi au hata matibabu ya maumivu madogo.

Hii yamaanisha kwamba yeyote anafika hospitalini bila shaka huwa ni azma yake kwamba achukue muda mfupi iwezekanvyo.

Je, hali ni ipi kwa wale wanaosalia hospitalini sio kwa siku, wiki kadhaa au miezi bali miaka na mikaka baada ya kuachwa kipweke hospitalini au kutelekezwa na jamaa zao?

Na hatimaye, baada ya kusalia kwenye wodi kwa miaka wao huishia wapi baada ya hospitali kufikia mwisho na kuwaondoa vitandani?

Duncan Khaemba amefanya pita pita zake katika hospitali ya taifa ya rufaa ya Kenyatta na kuandaa makala ya #JelaYaTiba.

« | »
News Features
||