Tetemeko la Musalia | Uamuzi wa Musalia kuungana na William Ruto

Imebainika kuwa Mwelekezo wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuwa viongozi wa One Kenya Alliance wasitishe azma zao za urais na kumuunga mkono Raila Odinga, kando na msimamo wa Odinga kuwa, iwapo si yeye, basi angempendekeza gavana wa zamani Wycliffe Oparanya kama mgombea urais, ndio uliokuwa chanzo cha mpasuko na tofauti zilizopelekea Musalia Mudavadi kuigura OKA na kuungana na William Ruto kwenye mrengo wa Kenya Kwanza. Miaka miwili kamili baada ya Musalia kufanya uamuzi huo alioutwika jina earthquake, na uliotikisa siasa za Kenya, mwanahabari wetu Ibrahim Karanja, ameirejelea siku hiyo, na kaandaa taarifa #TetemekoLaMusalia.
« | »
News Features