Ujasiri wa Monica

Huku mbari na ukoo wa Wamwere ukikaribiria kumzika mama wa jamii hiyo mwishoni mwa juma hili, kumbukizi za mama yao zitasalia kukita mizizi akilini mwao kila mara ukombozi wa pili wa taifa la Kenya unaposimuliwa.

Monica Wangu Wamwere, almaarufu Mama Koigi anakumbukwa kama mama jasiri na ngangari aliyepigana na serikali ya KANU kufa kupona kuilinda familia yake ambayo serikali ilikuwa imeikalia na uzito wake wote kiasi cha kuwaliza kila uchao.

Duncan Khaemba ameandaa makala maalum kugusia kwa kifupi tu tawasifu ya Mama Koigi.

« | »
News Features
||