Makala ya Chechemua: Daktari wa Madaktari Willy Amewaambia Viongozi Waache Siasa Wafanye Kazi

Wapo madaktari wa kila aina. Kuna wale wa kuchora mwelekeo wa siasa, kuna wale wataalamu wa elimu na kadhalika wapo wale wa afya. Mama Doro wa Riggy G anasema dawa ya kutibu uchumi ni kutoa wanaume ndani ya baa, nyuma ya baa na nje ya baa. Naye Daktari Alfred Mutua anayesimamia wanyamapori anasema fisi wanakula watu kwa sababu wamezaana sana na hawatosheki katika mbuga. Lakini waziri mwenzake wa afya daktari Suzy anasema anaogopa tiba ya mwanaume kutoka Ukambani. Anavyosimulia Papa Francis Mutegi katika makala mapya ya chechemua, daktari wa madaktari Willy amewaambia waache siasa wafanye kazi.
« | »
News Features