Fumbo La Gakuru

Marehemu gavana Patrick Wahome Gakuru alikuwa amehudumu kama gavana wa awamu ya tatu ya Nyeri kwa siku sabini na tisa pekee, kabla ya kukumbana na mauti kupitia ajali ya barabarani.

Wakati wa vikao vya mahakamani kutafuta ukweli kuhusiana na kifo chake cha kuogofya, mashahidi kadhaa  walisimulia jinsi gavana alishuhudia akiaga dunia baada ya kusalia amekwama ndani ya gari lake akiendelea kuvuja damu kwa wingi kwa zaidi ya dakika thelathini baadaye.

Familia yake ilijiondoa kwenye vikao hivyo baada ya kutofautiana vikali na mkurugenzi wa mashtaka ya umma alipopinga shinikizo lao la kuwataka watu fulani watano waitwe mahakamani ili wahojiwe. Je, hawa watano walikuwa ni akina nani? Mbona walikuwa na umuhimu sana katika vikao hivyo na kwa nini walikataa kufika kortini ili kujieleza na kumaliza shuku dhidi yao? Na pia je, ilikuwaje marehemu gavana akawa na polisi bandia kama mkuu wa ulinzi wake? Na kwa nini hadi wa leo kampuni ya bima kupitia kaunti ya Nyeri haijamlipa fidia aliyekuwa mlinzi wa Gakuru, Ahmed Kaib, manusura wa ajali hiyo ambaye alikatwa mguu wake mmoja? NTV inachunguza na kukuletea; Fumbo la Gakuru na Duncan Khaemba.
« |
News Features