Bugudhi Ya Hedhi

Katika ustaarabu wa kale  ulimwengu wa magharibi, maneno kama vile "laana," na "uchafu" yalikuwa maneno yaliyotumiwa kuelezea mzunguko wa hedhi. Haishangazi kwamba kwa miongo kadhaa, mchakato wa kawaida wa kibaolojia ambao wanawake wengi hupitia kila mwezi ulikabiliwa na ukandamizaji wa kijamii na kudhalilishwa kwa wasichana wadogo na wanawake . Athari za unyanyapaa huu pia zimeshuhudiwa nchini kenya, huku baadhi ya wasichana wakifikia hatua ya kujiua ili kuiepuka aibu ya hedhi. Ingawa hatua zimepigwa ili kukabiliana na aibu ya hedhi, jamii tulivu ya dasanach kaskazini mwa kenya bado imegubikwa kiza kiasi kwamba wasichana wengi wachanga wanahiari kupata ujauzito kama njia ya kuzuia hedhi. Ilichukua safari ya siku mbili kwa mwanahabari wetu mpekuzi ngina kirori na kikosi cha NMG kuifikia jamii ya dasanach kaunti ya marsabit ili kupata  simulizi hizi za kuvunja moyo.

« |
News Features