Fridah Mutheu Mwaka aka Kichuna
Fridah Mutheu Mwaka aka Kichuna
Mtangazaji wa Habari za Kiswahili, Habari
BIO

Najiamini kwa kuwa mwanamke mwenye tajriba na mmilisi wa fani ya uanahabari na mawasiliano. Safari yangu ya uanahabari iling’oa nanga rasmi mwaka wa 2016 kwenye kituo cha habari cha runinga ya EBRU na baadaye nikajiunga na kituo cha redio cha Kubamba FM na kisha nikafanikiwa kupanda ngazi za utangazaji kama mwanahabari mchanga wa runinga ya KTN News. Hapo nikawa mpeperushaji wa taarifa za KTN Leo na Wikendi, miongoni mwa taarifa nyenginezo.

Mwaka wa 2021 mlango wa riziki ulifunguka na ukurasa mpya nikaanza kuuandika kwenye ramani ya runinga ya NTV kama mwanahabari wa Kiswahili, Mhariri Msaidizi na Ripota wa masuala ya jinsia,uchumi na kijamii.

Tasnia hii imenipamba na tuzo za kitaifa na kimataifa. Kuu ikiwa ni mwaka wa 2023 nilipovikwa taji la kuwa mwanahabari bora wa kike Afrika kutoka nchi ya Accra, Ghana.(LIMAAWARDS)

Fursa ya kuzuru mataifa ya bara Afrika nimeikumbatia kwa ziara za kiuanahabari. La juzi ni mualiko niliouitikia kutoka Afrika Kusini katika kituo cha habari cha SABC.

Ni miaka tisa ya nyota za jaha, kurasa zilizojaa changamoto zilizonichonga na hata mema mazuri yanayonipamba.

Kiongeza Utamu

Kichuna likiwa ni jina langu la lakabu nilipambwa nalo kutokana na sanaa ya uimbaji. Nina vibao viwili vya nyimbo za injili. Mimi ni mlimbwende, vitenge na mishono ya aina yake navisuka. Ninalo duka la mishono – House of Kichuna.

Mila na desturi za kipwani zimenifunda kuwa mwanamke ng’ang’ari kwa hilo jikoni mie si mchache. Vidoho navipakua kisha kwa ustaarabu upo!!!

Read full bio

Recent by Fridah

see more link